Back to top

Wananchi Moro walalamikia ukosefu wa dawa kwenye maduka ya serikali.

19 July 2021
Share

Wananchi wa Manispaa ya Morogoro wameiomba serikali ya mkoa huo kufuatilia kwa undani sababu za maduka ya dawa kwenye hospitali za serikali kukosa dawa hivyo kuelekezwa kununua dawa kwenye maduka binafsi jambo linalowawia ugumu kutokana gharama kubwa za maduka hayo.
.
Akizungumza na ITV Mganga Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Kusirye Ukio, amekiri uwepo wa changamoto  ya wizi wa dawa kwa muda mrefu na kuahidi wapo mbioni kuipatia ufumbuzi huku Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela akiwataka viongozi wa wilaya zote  kulitazama jambo hilo kwa jicho kali kwani linahatarisha maisha ya wananchi.