Back to top

Wananchi vijijini waomba elimu ya vipodozi na vyakula vyenye madhara.

18 October 2018
Share

Wananchi waishio maeneo ya vijijini wilayani Mbinga mkoani Ruvuma wameiomba Mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) kuwapatia elimu ya vipodozi na vyakula vyenye madhara ili kujiepusha na   madhara ya vitu hivyo.

Wametoa rai hiyo katika maonyesho ya SIDO kanda ya nyanda za Juu Kusini yaliyofanyika wilayani Mbinga ambapo Meneja wa Chakula na dawa TFDA kanda ya Kusini Bw. Juma Bukuku anasema kuwa mamlaka hiyo imejipanga kupeleka elimu ya vipodozi vyenye madhara vijijini.