Back to top

Wananchi wa kijiji cha Nditi Nachingwea walia na Waziri wa Madini.

12 August 2019
Share

Wananchi wa kijiji cha Nditi halmashauri ya wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi wameiomba serikali  kuwapa idhini ya kuendelea kuchimba madini  yaliyopo katika mgodi wa Nditi wilayani humo, baada ya serikali kuwafutia leseni ya uchimbaji  wawekezaji waliokuwa wakichimba madini katika mgodi huo.

Wananchi hao wametoa kilio hicho mbele ya waziri wa madini, Mhe.Dotto Biteko alipopafanya ziara ya siku moja katika wilaya hiyo ambapo pamoja na mambo mengine  alitembelea mgodi huo wa Nditi na kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho

Kufuatia kilio hicho cha wananchi wa  kijiji cha nditi, 
wilayani nachingwea, mkoani lindi,waziri Biteko, amewaomba wananchi hao kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambapo suala lao likishughulikiwa kwa mujibu wa sheria.