Back to top

Wananchi walalamikia kutosomewa mapato na matumizi wilayani Shinyanga

14 November 2018
Share

Wananchi wa vijiji saba vinavyounda kata ya Lyabukande wilayani Shinyanga wamewalalamikia watendaji wa kata na vijiji kutowasomea mapato na matumizi tangu waingie madarakani miaka zaidi ya mitatu iliyopita na kudai kuwa wamekata tamaa ya kushiriki katika miradi ya maendeleo hali ambayo imesababisha mdororo wa maendekeo.
 
Malalamiko hayo yameibuka katika mkutano wa hadhara ulioshirikisha wananchi wa vijiji saba vinavyounda kata hiyo ambapo serikali imeombwa kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua watendaji hao kwa tuhuma za kuwanyima wananchi haki yao ya msingi.
 
Naye kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Bi.Beatrice Mwampunga amesema ni makosa wananchi kutosomewa mapato na matumizi na suala hilo inabidi lishughulikiwe kisheria huku mkuu wa wilaya hiyo Bi.Jasinta Mboneko akiwaagiza watendaji wa kata na vijiji kufikisha kwake taarifa ya mapato na matumizi ya fedha zilizochangishwa kwa wananchi kwa kipindi chote kinacholalamikiwa.