Back to top

Wananchi walalamikia mgogoro wao wa ardhi na hifadhi ya taifa Mahale

17 February 2019
Share

Wananachi wa kijiji cha Kalilani katika wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma ambacho kina mgogoro wa muda wa karibu miaka 35 na hifadhi ya taifa ya milima ya Mahale wamelalamika kukosa huduma za msingi na misaada toka serikalini na taasisi zake huku wakisisitiza kuwa eneo hilo ni lao na hifadhi wanatakiwa kuwaacha au kuwaondoa kwa kuwalipa fidia.
 
Wananchi hao wameiambia tume ya rais ya mawaziri wanane wanaotembelea maeneo mbalimbali nchini na kupendekeza hatua za kuchukua, kuwa wamechoshwa na mgogoro huo ambao unawafanya washindwe kufanya shughuli za maendeleo ambapo wameomba serikali kuwaachia eneo lililochukuliwa na hifadhi bila ridhaa yao huku uongozi wa hifadhi ya Mahale ukidai eneo hilo ni mali ya hifadhi.
 
kwa upande wake kiongozi wa tume hiyo ambaye pia ni waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Mhe.William Lukuvi amesema lengo la serikali ni kuona wananchi wanaishi kwa amani na Mhe. Rais John Magufuli licha ya kuagiza wananchi katika zaidi ya vijiji mia tatu nchini vyenye migogoro wasihamishwe, tume hiyo itatoa mapendekezo yatakayosadia kuboresha mahusiano na kumaliza kabisa migogoro.