Back to top

Wananchi walionunua mashamba yaliyofutiwa umiliki wake kubanwa.

17 May 2019
Share

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.William Lukuvi amesema wananchi wote walionunua kwa viongozi au bila kufuata utaratibu mashamba yaliyofutiwa umiliki wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli, hawatakuwa na haki kumiliki ya maeneo hayo kwani ni mali ya Serikali na hakuna mwenye mamlaka ya kuyagawa holela zaidi ya serikali kwa vigezo maalum.

Waziri Lukuvi amesema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Chanzuru Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro kwenye utambulisho wa Kikosi Kazi cha kupanga na kupima mashamba yaliyobatilishwa kwa Mkoa wa Morogoro kwa kuanzia na Wilaya ya Kilosa.