Back to top

"Wananchi wanataka uwanja mpya na si jengo la Kisasa" Dr Mwinyi

14 April 2021
Share

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr.Hussein Mwinyi amefanya ziara ya  ukaguzi wa ujenzi wa uwanja wa ndege mpya wa Zanzibar na kuwatahahdarisha wahusika kuwa wananchi wanataka kuona  uwanja wa kisasa na sio kuwa na jengo jipya pekee.
.
Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema ujenzi wa jengo jipya la Abiria (Terminal III), katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume unapaswa kwenda sambamba na utoaji wa huduma bora kwa wasafiri.

Aidha, Dk.Mwinyi, amesema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa ya ujenzi huo na kuwataka wasimamizi wa ujenzi kurekebisha mapungufu madogo madogo ili kuwa na uwanja wa kisasa na kuepuka hali iliyopo katika jengo la zamani.