Back to top

Wanaotumia jina la Rais Magufuli kujipatia kipato wanyooshewa kidole.

21 July 2020
Share

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Mara imesema baadhi ya watu wanatumia jina la Rais Dkt.John Pombe Magufuli kujipatia fedha, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu na kwamba zaidi ya shilingi milioni mia sita  zimekusanywa visivyo halali na viongozi hao kutoka kwa wafanyabiashara.

Mkuu wa TAKUKURU mkoani humo Alex Kuhanda amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwepo kwa baadhi ya viongozi wa serikali na Chama Cha Mapinduzi wanaotumia ambao wamekusanya kiasi hicho cha fedha visivyo halali kutoka kwa wafanyabiashara na wanasiasa mkoani mara.

Mkuu wa Mkoa wa Mara Bwana Adam Malima amesema baadhi wa watu wanaona kipindi cha uchaguzi kwao ni kipindi cha neema, hivyo amewataka wawe waangalifu kwani TAKUKURU ipo macho na itawabaini na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Wakati huo huo TAKUKURU mkoani Mara imefanikiwa kurejesha shilingi bilionni 1.5 zilizokuwa malipo hewa ya fidia kutoka mgodi wa North Mara  kwa vijiji vya Nyambichune na Matongo.