Back to top

Wanaovujisha taarifa binafsi za wateja wapewa onyo.

26 January 2021
Share

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe, Dkt. Faustine Ndugulile ametoa onyo kwa watoa huduma za mawasiliano nchini kuacha tabia ya kuvujisha taarifa binafsi za wateja kwa kuwadhibiti baadhi ya watumishi wao wasio waaminifu.
.
Ndugulile amebainisha hayo wakati akizungumza na watoa huduma za mawasiliano katika hafla ya kutia saini Mkataba baina yao na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) wa kupeleka huduma za mawasiliano katika vijiji 173 vilivyo katika mikoa 16 nchini.
.
Amesema kuwa hapendezwi na tabia ya baadhi ya watumishi wa makampuni hayo kuchapisha taarifa binafsi za wateja na kuzitoa kwa wagomvi wao na kwa watu wasio na nia njema.
.
“Niwaombe sana makampuni ya simu, someni vizuri sheria, vyombo vya dola ndivyo vinavyoruhusiwa kupata taarifa binafsi za mteja kwa malengo mahsusi na sio vinginevyo”,alisisitiza Ndugulile.
.
Ameongeza kuwa suala hilo atalisimamia kwa umuhimu wake na kampuni ya simu itakayotolewa malalamiko na wananchi kwa kuvujisha taarifa zao, hatua kali zitachukuliwa dhidi ya kampuni husika.