Back to top

Wanaume 10 wapotea Morogoro.

20 April 2019
Share

Watu 10 wote wakiwa wanaume wakazi wa vijiji tofauti vya kata ya Ruhembe wilaya ya kipolisi Ruhembe mkoani Morogoro, hawajulikani walipo baada ya kupotea kwa siku 18 sasa baada ya wananchi wa kijiji hicho kudai kuwa watu hao walikwenda kufanya shughuli za kibinadamu katika hifadhi ya taifa ya Mikumi kinyume cha sharia.

Tukio hilo la kupotea kwa watu hao limetajwa kutokea mnamo Aprili mbili mwaka huu baada ya watu hao kudaiwa kuingia kwenye hifadhi ya taifa ya mikumi na kisha kushindwa kurejea kijijini  hatua iliyopelekea wananchi kutoa taarifa kwenye vyombo vya usalama.

Kufuatia tukio hilo imemlazimu kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Wilbroad Mutafungwa kufika katika kijiji hicho nakuongea na wananchi kisha akawataka wananchi kuwa watulivu wakati jitihada za kuwatafuta  watu hao zikiendelea.