Back to top

Wanaume watakiwa kujitokeza kupima virusi vya UKIMWI.

23 July 2018
Share

Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi.Amina Masenza amewataka wanaume kujitokeza kupima maambukizi ya virusi vya Ukimwi ili kutambua kama wameambukizwa au laa na kuacha tabia ya kujificha nyuma ya migongo ya wanawake hali aliyoitaja kuwa haitoi picha halisi ya maambukizi hayo kwa wahusika.

Bi.Masenza amesema wapo wanaume ambao kwa kukosa ujasiri wa kujitokeza kupima hali yao ya Maambukizi ya vvu hutumia matokeo ya vipimo vya wake zao ama wapenzi wao kutambua hali zao jambo ambalo si sahihi.