Back to top

Wanawake wa kifugaji wapatiwa mafunzo ya kujikwamua kiuchumi.

24 May 2018
Share

Wadau wa Maendeleo wameanza kutoa elimu ya kuongeza thamani ya mazao yanayotokana na mifugo kama ngozi na maziwa kwa wajasiriamali wanawake kutoka jamii ya kifugaji katika wilaya ya Monduli ili mifugo waliyonayo iweze kuwakwamua kiuchumi.

Wadau wanatekeleza mpango huo katika taasisi ya maendeleo ya jamii Monduli ambapo zaidi ya wajasirimali wanawake miamoja  kutoka jamii ya kifugaji wamekusanyika kupata elimu hiyo.

Baadhi ya wajasirimali wanawake kutoka jamii ya kifugaji wanasema wamepata uelewa wa kutosha na sasa wapotayari kubadilika na kufanya ufugaji wenye tija kwa maendeleo yao.

Watafiti wa masuala ya maendeleo kwa jamii za kifugaji wanasema wanawake wa jamii hiyo wameshindwa kujikwamua kwakuwa wamesahaulika katika utatuzi wa shida zao ukilinganisha na jamii zingine.