Back to top

Wapiganaji wa MAIMAI wanaishambulia kambi ya kijeshi ya Congo.

21 September 2018
Share

Kambi ya kijeshi ya Congo DR iliyoko Mji wa Butembo Kivu kaskazini, Mashariki mwa nchi hiyo karibu na mpaka wa Uganda ambayo ndani yake kuna uwanja wa ndege wa Rughenda muda huu inashambuliwa na wapiganaji wa kundi la MAIMAI huku jeshi la nchi hiyo likisema kuwa katika majibizano ya uvamizi huo wamewaua wapiganaji kadhaa ambapo linaendela na msako kwa wapiganaji wengine ambao wamekimbilia katika makazi ya watu.

Wakati mapigano hayo yakiendelea madaktari wanaopambana kudhibiti ugonjwa wa Ebola katika eneo hilo wamesema wanakabiliwa na wakati mgumu wa kutoa huduma kutokana na mapigano yanayoendelea kwa sasa.