Back to top

"Wataalamu wafundisheni wananchi kufuga wanyamapori".Rais Magufuli.

03 January 2020
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa wito kwa Watanzania wengi zaidi kujitokeza kufuga wanyamapori kupitia bustani za wanyama (Zoo), ili kuongeza idadi ya wanyama hao na hivyo kupanua fursa za utalii na ajira.

Mhe. Rais Magufuli amewapongeza baadhi ya Watanzania walioanzisha Zoo hizo wakiwemo Lut. Jen Mstaafu Samwel Ndomba (Lugari Mini Zoo – Mbinga), Dar es Salaam Zoo, Bahari Zoo na wengine ambao wamefuga wanyamapori katika bustani na mashamba yao.

Amefafanua kuwa ufugaji wa wanyamapori unaruhusiswa kwa mujibu wa sheria ya wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009 na kwamba Watanzania wanayo haki ya kuwapata wanyamapori hao kwa mujibu wa sheria na taratibu, kuwafuga mahali popote panapofaa na patakapowezesha watalii wa ndani na nje ya nchi kutembelea.