Back to top

watakaoshiriki maandamano ya BAWACHA watahadharishwa.

09 May 2021
Share

Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma limewatahadharisha wananchi watakaojaribu kufanya maandamano yanayodaiwa kuratibiwa na Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) wilaya ya Geita yakidaiwa kuanzia Geita hadi Dodoma yakilenga kumshinikiza Spika wa bunge Mhe.Job Ndugai kuwaondoa bungeni wabunge 19 wa viti maalum CHADEMA kwa madai kuwa hawako bungeni kihalali, si halali na hayana nguvu za kisheria.
.
Akizungumza jijini Dodoma, Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Giles Muroto  amesema watakaokaidi na kufanya maandamano hayo, Jeshi la polisi litawawajibisha kwa mujibu wa sheria.
.
Aidha Kamanda Muroto amewataka wananchi kupuuza maandamano hayo huku akibainisha kuwa Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma liko imara kuwalinda wananchi na mali zao.