Back to top

Watanzania wameshauriwa kujenga mazoea ya kutembea na nyaraka muhimu.

07 December 2018
Share

Watanzania wameshauriwa kujenga mazoea ya kutembea na nyaraka zote muhimu za utambulisho wao pindi wanapokuwa safarini ili kurahisisha mawasiliano wakati linapotokea jambo lolote linalohitaji mawasiliano ya dharura.
 
Wito huo umetolewa na Afisa ustawi wa jamii kutoka hospitali ya rufaa ya Kibena mkoani Njombe bwana Samson Sollo wakati akizungumza na vyombo vya habari juu ya mkazi wa mmoja wa Songea aliyefahamika kwa majina ya George Lutuhi ambaye amefariki akiwa anapatiwa matibabu na hakuna ndugu aliyejitokeza hadi sasa na wala hakuwa na taarifa zozote amazo zingesaidia kuwapata ndugu zake.

Amesema marehemu baada ya kuugua alifikishwa hospitalini hapo Disemba Mosi ya mwaka huu akitokea katika nyumba ya kulala wageni ya Iditima iliyopo mjini Njombe eneo alilofikia kabla ya kuelekea Mtera huko mkoani Iringa kwenye shughuli za uvuvi.

Dokta Melele Anasema Kwa Mujibu wa Taratibu Ndugu Wasipopatikana Katika Kipindi Cha Siku 14 Kuchukua Mwili Huo Basi Serikali Italazimika Kuuzika.