Back to top

Watanzania wang’ara Nagai Marathon nchini Japan

21 October 2018
Share

Wanariadha watanzania wameng’ara katika Nagai Marathon huku wanariadha wake wakiongoza katika full marathon na half marathon

Katika full marathon kwa wanaume Marco Joseph amemaliza Nafasi ya kwanza  akitumia saa 02 :21:13 huku mtanzania mwingine Willbaldo Peter akimaliza nafasi ya pili na kwa wanawake Angel John ameshika nafasi ya kwanza akitumia muda wa  02:43:21

Katika half marathon mwanariadha mzoefu Fabian Joseph amemaliza Nafasi ya kwanza akitumia saa 01:02:53 na kwa wanawake Amina Mohamedi akimaliza wa kwanza akitumia muda wa saa 01:16:08 huku watanzani wengine wakishika nafasi ya pili mpaka ya tano