Back to top

Watanzania watahadharishwa juu kuwepo kwa tishio la ugonjwa wa Ebola.

15 June 2019
Share

Serikali kupitia Wizara ya afya ,maendeleo ya jamii, jinsia,wazee na watoto imetoa tahadhari juu ya kuwepo kwa tishio la mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini.

Mikoa ya Kagera,Mwanza na Kigoma yatajwa kuwa katika hatari zaidi kutokana na mwingiliano mkubwa na nchi ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo pamoja na  nchi ya Uganda ambazo zimeripotiwa kuwa na vifo vya wagonjwa wa Ebola.

Waziri Ummy Mwalimu ametembelea uwanja wa ndege wa Mwanza ili kujionea wanavyoweza kukabiliana na wasafiri wenye dalili za ugonjwa huo.

Kufuatia kuwepo kwa tetesi ya mtu mmoja mkazi wa Kitangiri jijini Mwanza kudaiwa kufariki kwa ugonjwa wa Ebola na ndugu zake saba kulazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza sekou toure,Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo dokta bahati msaki amedai watu hao walikula chakula chenye sumu.