Back to top

Watatu wafariki kwa kugongwa na gari ya askari wa TANAPA.

16 June 2020
Share

Watu watatu  wakazi wa Kijiji cha Mamire wilayani Babati mkoani Manyara waliokuwa wakisafiri kwa kutumia  bodaboda wamefariki duniani papo hapo baada ya kugongwa na gari la Askari wa Wanyamapori wa  Hifadhi ya Taifa ya Tarangire(TANAPA) waliokuwa doria katika eneo la kijiji hicho linalopakana na hifadhi hiyo.


Kamanda wa polisi mkoani Manyara Paul Kasabago amesema ajali hiyo  imelihusisha gari aina ya Toyota Land Cruiser namba SU 417 mali ya TANAPA linaloshikiliwa katika kituo cha polisi Babati baada ya dereva wake kulitelekeza na kutoweka baada ya kuigonga pikipiki  iliyokuwa ikiendeshwa na Aaidi Alli ambaye amefariki dunia.