Back to top

Watendaji wa idara ya ardhi nchi watakiwa kufanya kazi kwa uadilifu.

11 July 2019
Share

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi.Dorothy Mwanyika amewataka watendaji wa idara ya ardhi nchi kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu mkubwa katika kuwahudumia wananchi.

Bi. Mwanyika amesema watendaji wa idara ya aridhi katika maeneo mbalimbali hapa nchini wamekuwa wakilalamikiwa na kwamba sehemu kubwa ya migogoro inachangiwa na watumishi hao.

Katibu Mkuu huyo ameyasema hayo Mjini Lindi, wakati akizungumza na watumishi wa idara zilizo chini ya wizara yake pamoja wakurugenzi wa halmashauri.

Amesema kuna maeneo mengine utakuwa watu wanadhulumiwa haki zao ambapo mkoa wa Dar Es Salaam umezidi kwani utakuta mtu amejenga nyumba yake mara anashtukia nyumba inauzwa, na anashangaa inauzwa wakati hajawahi kukopa benki hata siku moja lakini anaambiwa nyumba yake ina mkopo zipo kesi za hivyo.

Hivyo watumishi wanatakiwa kuwa waadilifu katika kutekeleza majukumu yao ya kikazi kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma.