Back to top

Watoto wanaopelekwa kliniki kuchunguzwa kama wamefanyiwa ukeketaji.

13 June 2018
Share


Maadhimisho ya Siku ya mtoto wa Afrika yamefanyika kitaifa hii leo jijini Arusha na kuhudhuriwa na watoto,Mashirika ya kimataifa yanayo jishughulisha na masuala ya watoto pamoja na wadau mbalimbali ambapo katika Maadhimisho hayo serikali imesema kuwa imejipanga kuhakikisha inakomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuwataka watoto kutokaa kimya wanapopata kadhia hiyo.

Akizungumza katika Maadhimisho hayo Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii,jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu katika hotuba yake iliyosomwa na Naibu Waziri wake Dakta Faustine Ndungulile amesema kuwa baadhi ya mikakati iliyo wekwa na serikali ni pamoja na kuwachunguza watoto wanaopelekwa kliniki kama wamefanyiwa ukeketaji kutokana na kuzuka kwa tabia hizo kwa baadhi ya wazazi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Joel Festo amezitaja changamoto mbalimbali zinazowakabili watoto na kuwakilisha maadhimio yao katika mabaraza wanayokaa ikiwemo kutoachwa nyuma katika uchumi wa viwanda na haki ya mtoto kusikilizwa.


Nao baadhi ya wadau wa masuala ya watoto likiwemo Shirika la kimataifa la watoto-UNICEF wamehaidi kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuhakikisha kuwa haki za mtoto zinazingatiwa ikiwemo masuala ya elimu na afya.