Back to top

Watu 10 wamejeruhiwa katika ajali Mlima Kitonga mkoani Iringa.

16 October 2018
Share


Watu kadhaa wamenusurika kifo katika mlima Kitonga Mkoani Iringa  baada ya basi la kampuni ya New force lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Dar es Salam kugongana na gari nyingine linalodaiwa kuwa ni la kampuni ya Golden deer lilokuwa likitokea  Dar Es salaam kuelekea Tunduma. 

Akiongea kwa njia ya simu na ITV Online kamishna msaidizi wa polisi Deusdedit Kasindo ambaye pia ni kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa amesema watu 10 wamejeruhiwa katika ajali hiyo, wanne kati yao ni wanaume , wanawake 5 na mtoto mmoja wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya mwaka mmoja na nusu na miwili ambapo wawili kati yao hali zao si nzuri na wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa wakati majeruhi wengine wanapata matibabu katika Hospitali ya Wilaya Ilula.