Back to top

Watu 12 Mtwara wagundulika na ugonjwa wa homa ini.

17 July 2019
Share

Serikali ya mkoa wa Mtwara imesema watu kumi na mbili wamebainika kuwa na ugonjwa wa homa ya ini hivyo imewataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo ambao upo katika wilaya ya Nanyumbu na Newala.

Akizungumza katika kikao cha ushauri cha mkoa Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni mkuu wa mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa amesema ugonjwa huo umepatikana kwa vijana walioomba kujiunga na Jeshi la kujenga taifa mara baada ya kufanyiwa vipimo.

Amesema vijana hao kumi wamebainika kutoka wilaya Nanyumbu huku wagonjwa wawili wakibainika kutoka wilaya Newala wote katika mkoa wa Mtwara.