Back to top

watu 14 wafariki ajalini katika eneo la Dundani wilayani Mkuranga

25 June 2018
Share

Watu 14 wa familia moja wamefariki na wengine 4 wamejeruhiwa baada ya Gari dogo aina ya Toyota Hiace kugongana uso kwa uso na Lori la Mchanga lenye namba za usajili T 439 DCC  katika kijiji cha Dundani wilayani Mkuranga.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Rufiji, Onesmo Lyanga akizungumza na ITV/Radio One kwa njia ya sumu amesema chanzo cha ajali ni dereva wa Lori alikuwa amesinzia.

Kwa upande wake mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Dkt.Steven Mwandambo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na zoezi linaloendelea kwa sasa ni kuwanasua baadhi ya majeruhi walionasa katika magari hayo.

Ajali hiyo imetokea wakati watu hao wakielekea katika shughuli za Mahafali ya JKT Msata Kambi Kihangaiko ambapo watu wa familia moja walikodi Hiace hiyo iliyogongwa na lori number T439 DCC aina ya Scania iliyokuwa inaenda kubeba Mchanga.