Back to top

Watu 127 wamepoteza maisha katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere.

21 September 2018
Share

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema kufuatia ajali ya kivuko cha Mv Nyerere iliyotokea Mkoani Mwanza  mpaka sasa  jumla ya watu 127 wamepoteza maisha huku wengine 40 wakiokolewa .

Balozi John Kijazi ameongeza kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kivuko hicho kilibeba abiria zaidi ya uwezo wake na kwamba kuanzia kesho bendera ya Taifa itapepea nusu mlingoti kama ishara ya kuomboleza msiba kwa siku tatu.