Back to top

Watu 3 wa familia moja wamefariki baada ya kugongwa na gari Handeni.

21 May 2018
Share

Ajali hiyo imetokea majira ya saa kumi jioni katika eneo la kijiji cha Bogolwa nje kidogo ya mji wa Handeni ambapo gari ndogo yenye namba za usajili T 865 AWF ambalo lilikuwa likitokea Mkata kwenda Handeni lilihama njia na kuwagonga watu hao ambao ni wa familia moja waliokuwa wakitokea shambani baadhi ya mashuhuda wanaelezea hali ilivyokuwa. 

Baadhi ya viongozi mbali mbali ambao wamefika kwenye tukio hilo wameeleza kusikitishwa kwao na tukio hilo huku baadhi yao wakiwaomba madereva kuzingatia kanuni na sheria za usalama barabarani. 

Mpaka sasa majeruhi watatu wamefikishwa kwenye hospitali ya wilaya Handeni kwa ajili ya matibabu.