Back to top

Watu 3 wanaosadikiwa kuwa majambazi wameuawa kwa risasi Mwanza

06 February 2019
Share

Jeshi la polisi mkoani Mwanza limewaua kwa risasi watu watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi katika mtaa wa Nyakabungo jijini Mwanza wakati wakijiandaa kuvunja  maduka yaliyopo kwenye mtaa huo.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, kamishna msaidizi wa polisi Advera Bulimba amesema majambazi hao baada ya kuhisi uwepo wa polisi katika mtaa huo, walianza kujihami kwa kuwarushia askari risasi.

Tukio la kuuawa kwa majambazi hao limekuja katika kipindi kisichozidi wiki mbili, baada ya watu wengine nane wanaosadikiwa kuwa majambazi kuuawa wilayani Ukerewe januari 26 mwaka huu katika majibizano ya kurushiana risasi na askari polisi katika eneo la daraja linalotenganisha kijiji cha Igalla na Buhima pamoja na kwenye mapango ya mlima wa kijiji cha Lutare.