Back to top

Watu 44 wapoteza maisha katika jimbo la Califonia nchini Marekani

13 November 2018
Share

Watu 44 wamepoteza maisha katika jimbo la California nchini Marekani baada ya moto kuzuka huku kazi ya kusaka  miili kwenye mabaki ya moto huo ikiendelea.

Taarifa za mamlaka za california zinasema kuwa inaonekana watu waliofia kwenye magari yaliyokuwa yameegeshwa walikuwa katika harakati za kuwahi kuondoka eneo la tukio lakini hawakufanikiwa kutimiza ndoto zao hizo.

mpaka sasa inaelezwa mamia ya watu hawajulikani walipo baada ya kuzuka kwa moto huo.