Back to top

watu 5 wafariki baada ya basi kugongana na lori Morogoro.

16 August 2019
Share

Watu watano wamefariki na wengine 26 wamejeruhiwa baada ya basi la abiria la Safari njema kugongana uso kwa uso na lori aina ya tata mali ya kiwanda cha Tumbaku cha Alliance One katika eneo la Nanenane manispaa ya Morogoro.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa saba usiku ambapo majeruhi 26 akiwemo mtoto mdogo wameshakimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Manispaa ya Morogoro na wanaendelea na matibabu.