Back to top

Watu 6 mbaroni kwa uhalifu akiwemo anayetuhumiwa kubaka wanawake.

14 September 2018
Share

Jeshi la polisi mkoani Mwanza limewakamata watu sita wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya uhalifu katika matukio mbalimbali mkoani humo pamoja na mikoa ya jirani ya Kanda ya Ziwa akiwemo Mfanyabiashara na Mkazi wa Dar es Salaam Kennedy Obworo, anayetuhumiwa  kuhusika na matukio ya kuwanyeshwa dawa za kulevya wanawake na kisha kuwabaka katika mikoa ya Dar es Salaam, Geita, Mara, Arusha na Mwanza.

Kamishna Msaidizi wa Polisi Jonathan Shanna amesema miongoni mwa watuhumiwa yumo mkazi wa kijiji cha Isangijo wilayani Magu Sheshe Bomani ambaye ni Mganga wa jadi anayetuhumiwa kumiliki nyara za serikali kinyume cha sheria kwa madai ya kujihusisha na upigaji wa ramli chonganishi.