Back to top

Watu 71 wanusurika kifo kwa kunywa togwa kwenye sherehe.

21 September 2020
Share

Watu 71 wa kijiji cha Liula wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, wamenusurika kifo baada ya kunywa kinywaji aina togwa kinachodhaniwa kuwa na sumu wakiwa kwenye moja ya sherehe ya kidini maarufu kama sadaka.

 Mkuu wa wilaya ya Songea, Bw.Pololeti Kamando Mgema amepiga marufuku matumizi ya togwa kwenye sherehe zote wilayani humo kutokana na matukio hayo kujirudia rudia.
 
Nao baadhi ya wananchi wa kijiji cha Liula Songea waliokumbwa na kasumba hiyo wamesema baada yakunywa kinywaji hicho   hali ilianza kubadilika kwa kuanza kuarisha na kutapika.