Back to top

Watu 9 wanashikiliwa na polisi Mbeya kwa tuhuma za mauaji ya askari.

11 October 2018
Share

Wananchi jamii ya wafugaji wamewashambulia na kuwaua askari wawili wa Shirika la hifadhi za taifa,TANAPA, katika hifadhi ya taifa ya Ruaha wilayani Mbarali na kisha kupora silaha moja iliyokuwa na askari hao.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Urlich Matei amesema tukio hilo limetokea jana wilayani Mbarali ambapo hadi hivi sasa watu tisa wanashikiliwa na polisi wakihusishwa na tukio hilo, na kwamba silaha iliyoporwa imepatikana.