Back to top

Watu milioni 470 ulimwenguni kote hawana ajira.

21 January 2020
Share

Watu milioni 470 ulimwenguni kote hawana ajira kabisa au hawana kazi nzuri ya kuwawezesha kujenga mustakabali bora,kwa mujibu wa ripoti ya kila mwaka ya Shirika la Kazi Duniani ILO.

Kwenye ripoti ya UN ya kila mwaka kuhusu ajira na tathmini ya jamii, Shirika la Kazi Duniani, ILO, limesema Mwaka huu, idadi ya watu ambao wamesajiliwa kuwa hawana ajira inatarajiwa kuongezeka kutoka milioni 188 mwaka uliopita hadi milioni 190.5.