Back to top

Watu wanne mbaroni kwa kukutwa na noti bandia za zaidi ya nchi 12.

18 January 2019
Share

Jeshi la  polisi mkoani  Arusha linawashikilia  watu wanne wanaohusishwa  na mtandao wa kimataifa wa  kutengeneza noti bandia ambao  wamekamatwa wakiwa na maelfu ya noti  bandia za nchi zaidi ya 12 zikiwemo  dola  za Kimarekani , Euro  na fedha nyingine.

Kamanda wa polisi  wa mkoa wa Arusha Bw  Ramadhani Ng'anzi amesema   watuhumiwa hao wanaoendelea kuhojiwa  pia wamekutwa na mashine na baadhi ya vifaa  vya kutengeneza fedha hizo bandia wakiwa wameshatengeneza  kiasi kikubwa cha fedha za nchi mbalimbali .