Back to top

Watu wanne wakutwa na maambukizi ya COVID-19 kambi ya wakimbizi Suda

14 January 2021
Share

Mashirika ya misaada yaliripoti watu wanne kukutwa na  COVID-19 katika kambi ya Um Rakouba ya Sudan kwa wakimbizi wa Ethiopia wiki hii. Kambi hiyo ni makazi ya watu 25,000 ambao wamewasili tangu novemba mwaka jana

Wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu wiki hii wamethibitisha maambukizi hayo  katika kambi za Sudan kwa wakimbizi waliokimbia mapigano katika mkoa wa Tigray nchini Ethiopia. Shirika la kuhudumia wakimbizi katika Umoja wa Mataifa-UNHCR na kundi la msaada la Mercy Corps wanasema uingiliaji wa haraka unahitajika ili kuepusha janga la kibinadamu.
 

VOA