Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimethibitisha kupoteza watu wanne kati ya watano waliohusika kwenye ajali ya gari la wagonjwa kugongwa na lori eneo la Riverside Ubungo jijini Dar es salaam jana usiku.
Taarifa ya Makamu Mkuu wa Chuo hicho prof. William Anangisye kwa vyombo vya habari imesema ajali hiyo imetokea wakati gari la wagonjwa wa chuo likiwakimbiza wanafunzi wawili kutoka zahanati ya Mabibo kwenda kituo cha afya cha Chuo kikuu kwa matibabu zaidi.
Waliopoteza maisha ni pamoja na dereva mwandamizi wa gari la wagonjwa James Josephat, muuguzi msaidizi Jonathan Bashuda,mwanafunzi wa mwaka wa pili Erasto Sango na mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Mary Godian.
Mwanafunzi mwingine Nkiko Abishai wa mwaka wa tatu alijeruhiwa na kulazwa hospitali ya Muhimbili akiendelea kupokea matibabu.
Mwenyezi mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi amina.