Back to top

Watu watatu wamekamatwa wakijifanya watoza ushuru mkoani Mbeya.

09 January 2019
Share

Jeshi la polisi mkoani Mbeya kwa kushirikiana na maofisa wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya limewakamata watoza ushuru feki watatu ambao walijifanya ni maofisa wa halmashauri hiyo na kukusanya ushuru kutoka kwenye magari yanayosafirisha mazao ya nafaka na misitu kwa zaidi ya miezi sita na kuisababishia serikali hasara ya mamilioni ya fedha.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, kamishna msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi Ulrich Matei amesema watuhumiwa hao wamekamtwa wakiwa kwenye mizani ya magari katika eneo la uyole jijini mbeya wakiendelea na ukamataji wa magari kinyume na sheria ikiwa ni baada ya kuwekewa mtego na jehi la polisi kwa kushirikiana na maofisa wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya.

Aidha kamanda Matei amesema,uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa watuhumiwa hao walishawahi kukamatwa na kufikishwa mahakamani ambako walihukumiwa kifungo cha nje na kutakiwa wasifanye kosa lolote mpaka watakapomaliza kifungo chao, lakini wameendelea kujihusisha na vitendo hivyo vya kiharifu.

Afisa masuhuri wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya  Mapakani Kalinga amewaomba wananchi wanapotakiwa kulipa malipo yoyote ya serikali wahakikishe wanapewa stakabadhi ya kielektroniki ili kuepuka matapeli.