Back to top

Watu wawili wamefariki dunia kwa kusombwa na maji Ruvuma

21 February 2020
Share

Watu wawili wamefariki dunia katika kata ya Matumbi halmashauri ya wilaya ya Madaba mkoani Ruvuma kwa kusombwa na maji  ya mto huku baadhi ya  barabara na madaraja yakiathirika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Diwani wa kata ya Matumbi Bw.Valentine Mtemauti amesema mito kwenye kata yake imefurika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha ambapo mkazi wa kata hiyo Shomari Saidi amesombwa  na maji ya mto Luhuji  na kupoteza maisha huku barabara ya Madaba-Ifinga ikiharibika na kukaribia kukatika


Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi.Christina Mndeme amewataka wananchi kuchukua tahadhari kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.