Back to top

Watu wenye Ualbino wakemea imani potofu dhidi yao kulekea uchaguzi.

13 June 2020
Share

UKEREWE MKOANI MWANZA

Chama cha Watu wenye Ualbino wilayani Ukerewe mkoani Mwanza kimeadhimisha Siku ya Kukuza Uelewa Kuhusu Ualbino Duniani kwa kuviomba vyombo vya dola vidhibiti mauaji na vitendo vya ukatili dhidi yao katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani.

Watu 50 wenye Ualbino wilayani humo wametoa ombi hilo katika mkutano wao katika kituo cha mafunzo ya ufundi cha Bukongo wilayani Ukerewe kutafakari hali yao ya baadaye wakati wa uchaguzi huo.

Katibu wa Chama cha Waganga wa Tiba Asilia na Wakunga wilaya ya Ukerewe, Maneke Keya, akizungumza katika maadhimisho hayo kuwaonya kuonya na kuwakemea baadhi ya waganga wasio waaminifu.

Katibu Tawala wa wilaya ya Ukerewe, ambaye pia ni mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya Chama cha Watu Wenye Ualbino wilayani humo Bwana Focus Majumbi amesema serikali haitawafumbia macho waganga wa tiba za asili wanaoendeleza vitendo vya uvunjifu wa amani.

Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Kukuza Uelewa Kuhusu Ualbino Duniani mwaka huu ni Haki Sawa kwa Wot, Boresha Afya, Elimu na Ajira kwa Watu Wenye Ualbino.