Back to top

Watu zaidi ya 300 wanatafutwa na Polisi Kagera kwa tuhuma za uvamizi.

10 January 2019
Share

Jeshi la polisi katika mkoa wa Kagera linawasaka watu zaidi ya 300 wa kijiji cha Kilela kilichoko wilayani Kyelwa waliokuwa na silaha za jadi ambao wanahusika na tuhuma ya kuwavamia wananchi wa kijiji cha Kibingo kilichoko wilayani humo na kuchoma nyumba 16 za wananchi wa kijiji hicho pamoja na kuharibu mali zilizokuwa mashambani.  

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Kagera Kamishina Msaidizi, Revocatus Malimi amesema watu hao walivamia kijiji cha Kibingo kwa lengo la kuwasaka watu wanaotuhumiwa kuhusika na tukio la mauaji ya kikatili ya mwendesha bodaboda, Albert Antipas.