Back to top

Watuhumiwa 12 wa utoroshaji wa madini wafikishwa mahakamani Mwanza.

13 March 2019
Share

Watuhumiwa 12 wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 3 ya mwaka 2019 ya utoroshaji wa madini ya dhahabu yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 27 kwa mara ya tatu hii leo wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mwanza.

Hii ni baada ya Februari 25 mwaka huu kushindwa kutokea mahakamani hapo kwa madai ya mvua kunyesha, huku ulinzi mkali wa askari polisi wenye silaha za moto na mabomu ya machozi ukiwa umeimarishwa kuzunguka viwanja vya Mahakama kuu kanda ya Mwanza.