Back to top

Watumishi hewa walipwa mishahara Tanga

23 May 2018
Share

Serikali mkoani Tanga imewaagiza wakuu wilaya na wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha kuwa wanawachukulia hatua kali za kisheria baadhi ya watendaji wao baada ya kubaini kuwa baadhi yao wanapokea mishahara ya watumishi hewa waliostaafu huku wengine wakiwa wamefariki dunia na kuzorotesha zoezi la Mheshimiwa rais Dkt.John Pombe Magufuli la kukabiliana na matumizi mabaya ya fedha za serikali. 

Akizungumza na viongozi wote wa serikali za mkoa wa Tanga mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigella amesema inastaajabisha baadhi ya mishahara hiyo bado inaendelea kutumika halafu watendaji husika wanashindwa kuchukua hatua kali za kisheria hivyo ni lazima fedha hizo zirudishwe.

Aidha amesema wamebaini kuwa bado wapo baadhi watendaji wa halmashauri ambao wanakusanya maduhuli ya serikali wanadaiwa kuficha vitabu vya makusanyo hatua aliyoielezea kuwa ni yenye ishara ya hujuma.

Kufuatia hatua mkurugenzi halmashauri ya wilaya ya Muheza Luiza Mlelwa amekiri kuwepo kwa mishahara hewa inayoingizwa kwenye benki wanazochukua mishahara watumishi na wamejaribu kuwaandikia viongozi wa benki ili kurudisha fedha hizo makao makuu hazina lakini hadi sasa ameshindwa kujibiwa.