Back to top

Watumishi wawili wasimamishwa kazi Bunda.

12 June 2021
Share

Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Bunda mkoani Mara, limewasimamisha kazi watumishi wake wawili, huku likisema halina imani na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Amos Kusaja kwa tuhuma za kushindwa kusimamia mapato ya Halmashauri na kusababisha upotevu wa mamilioni ya fedha za walipa kodi. 

Watumishi waliosimamishwa kazi ni Mweka hazina wa Halmashauri hiyo Shaban Ndalo pamoja na Afisa Manunuzi Allan Aron.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bunda Charles Manumbu amewataka watumishi wa halmashauri hiyo kuepuka kujiingiza kwenye mikataba mibovu, huku Katibu tawala wa wilaya ya Bunda Salum Mtelela naye akitoa angalizo kwa watendaji na madiwani wa Halmashauri hiyo.