Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amewasimamisha kazi wauguzi wanne wa kituo cha afya Mkoani wilaya ya Kibaha mkoani Pwani ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazowakabili kutoa lugha chafu kwa mama aliyempeleka mwanaye kituoni hapo kupatiwa matibabu na kuamua kukimbilia hospitali nyingine.
Akizungumzia uamuzi huo mara baada ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya elimu ujenzi na afya kikiwemo kituo cha afya cha Matibwa Bagamoyo Mhandisi Ndikilo amesema alipokea malalamiko ya mama huyo kufika hospitalini hapo hali ya mtoto ikiwa mbaya lakini wauguzi walishindwa kumsaidia licha ya kuwaomba badala yake kuambulia lugha za kejeli na kuagiza miundombinu bora ya ujenzi wa vituo kama hivyo uende sambamba na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.