Back to top

Wavuvi watakiwa kuzingatia sheria na taratibu mkoani Lindi.

29 September 2020
Share

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama, Mahmoud Kimbokota amewataka wavuvi Mkoani Lindi kuzingatia Sheria na taratibu zinazo simamia uvunaji wa rasilimali za Bahari.

Kimbokota amesema hayo alipokutana na timu ya Wataalamu wa Mradi wa Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Bahari Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOfish) walipokwenda kufanya ufuatiliaji na kutathimini maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtama, Mkoani Lindi.

Akitoa taarifa ya maendeleo ya mradi wa SWIO fish, Kimbokota amesema kuwa wavuvi wanatakiwa kutambua kuwa uvuvi ni shughuli rasmi ya kujipatia kipato kama zilivyo shughuli nyingine, hivyo ni lazima waiheshimu na kuithamini.

Kimbokota ameishukuru serikali kwa kupeleka mradi huo wilayani humo na kusema kuwa jamii imeanza kubadilika, huku akiiomba Serikali kuendelea kuwawezesha wavuvi ili waweze kukuza mitaji yao na kupata zana za kisasa na kuachana na matumizi ya zana za kienyeji.

Kimbokota ameongeza kuwa kutokana na uboreshwaji wa usimamizi wa rasilimali uliofanywa na mradi hususani katika eneo la doria, wavuvi wameanza kufuata sheria na taratibu na umesababisha kudhibitiwa vizuri kwa mapato ya Halmashauri.