Back to top

Wawekezaji wawekewa mazingira rafiki ya uwekezaji Nyasa.

16 December 2019
Share

Serikali Mkoani Ruvuma imesema imeweka mazingira mazuri kwa wawekezaji ili kuvutia zaidi uwekezaji na kuwataka wawekezaji kuwekeza  katika sekta ya utalii katika Wilaya ya Nyasa yenye vivutio vingi vya utalii na fursa nyingi za utalii.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Bi.Christina Mndeme amesema Wilaya ya Nyasa ina vivutio vingi vya utali na amewakaribisha wawekezaji katika sekta ya utali kuwekeza katika wilaya hiyo yenye vivutio vingi vya utalii likiwemo Jiwe la Pomonda lililoko katika Ziwa Nyasa.