Back to top

Wawili wahukumiwa kifungo cha miaka sita au faini ya Mil.12

12 September 2018
Share

Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu imewahukumu kifungo  cha miaka sita au faini ya shilingi Milioni 12 kila mmoja na kutaifisha madini yote baada ya kukubali makosa ya kuongoza uhalifu wa kupanga na kukutwa na madini kinyume cha sheria kwa washtakiwa wawili  Bw.Aazam Nazim na  Bw.Ango Mbossa baada ya kukamatwa na madini ya Rough Gestone yenye thamani ya bilioni 4.

Akitoa maamuzi hayo  Hakimu Mkazi mwandamizi Agustine Rwizile amesema kutokana maelezo ya pande zote mbili utetezi na serikali na kwa kuzingatia hilo ni kosa la kwanza kwa washtakiwa hao mahakama imeamua kutoa hukumu hiyo ili iwe fundisho kwao na wananchi wengine.