Back to top

Wawili wapoteza maisha Kagera kwa kufunikwa na kifusi na kupigwa na ra

11 December 2018
Share

Mkazi wa kijiji Kalagenda wilayani Ngara mkoani Kagera Robert Jacob ambaye ni mkulima amepoteza maisha baada ya kupigwa na radi iliyoambatana na mvua kubwa yenye upepo mkali wakati akiwa pembezoni mwa nyumba yake akikinga maji ya mvua .

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Kagera Kamishina msaidizi Revocatus Malimi amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo na katika tukio hilo amewataja watu wawili waliojeruhiwa na radi hiyo ambao wamelazwa katika hospitali teule ya wilaya ya Ngara ya Omulugwanza kuwa ni pamoja na Yamungu Robert mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Bulukulungo na Mapinduzi Jacob ambaye ni mkazi wa kijiji cha Kalagenda.  

Kamanda Malimi amesema tukio jingine la kifo lililotokea mkoani humo ni lile la mkazi wa kijiji cha Rwenkungo kilichoko katika kata ya Kabindi wilayani Biharamulo Paul Nyerere amepoteza maisha baada ya kufukiwa na kifusi cha mchanga wakati akitafuta mchanga kwa ajili ya kujenga nyumba yake.