Back to top

Wazazi Butiama wadaiwa kuwakeketa wanafunzi wa kike nyakati za usiku  

04 December 2018
Share

Imebainika kuwa kuna idadi kubwa ya wanafunzi wa kike wa shule za msingi na sekondari katika tarafa ya Kiagata wilayani Butiama mkoani Mara tayari wamefanyiwa vitendo vya ukeketaji nyakati za usiku katika msimu huu wa ukeketaji, huku wengine wakiwa tayari wameandaliwa kufanyiwa vitendo hivyo mapema mwezi huu.
 
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu maalum ya kutoa elimu mashuleni katika kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia,likiwemo tatizo kubwa la ukeketaji watoto wa kike,mkurugenzi mtendaji wa shirika la Matumani kwa wasichana na watoto wa kike Bi.Robhi Samwel,amesema wamebaini hivi sasa kuna idadi kubwa ya watoto wa kike ambao tayari wamefanyiwa vitendo hivyo vya kikatili.