Back to top

Wazazi wadaiwa kuchochea ukatili wa kijinsia Songwe.

16 June 2018
Share

Mfumo wa maelewano baina  ya wazazi na watuhumiwa wa vitendo vya ukatili dhidi watoto maarufu kama "kuyamaliza chini kwa chini" umedaiwa kuchochea ongezeko la ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto katika maeneo mbalimbali mkoani Songwe, kutokana wazazi kuficha taarifa mhimu ili kukwamisha hatua za kisheria kuchukuliwa.

Baadhi ya wazazi walioshiriki Maadhiisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika kimkoa katika uwanja wa mbozi Mission mkoani songwe, wamesema mfumo huo umeshamiri sana maeneo ya vijijini na kueleza madhara yake.

Afisa Maendeleo ya jamii mkoa wa Songwe Bi.Gift Sichone amedai kuwa ongezeko la vitendo vya ukatili wa kijinsia kimkoa umeongezeka kwa kiasi kikubwa kutokana na wazazi kukubaliana kwa siri na watuhumiwa wa ukatili ili kukwepa mkono wa sheria.

Jumla ya mashauri 118 ya ukatili wa kingono dhidi ya watoto wa kike yameripotiwa kwa kipindi cha mwezi Januari hadi MachI 2018 tofauti na mwaka jana 2017 ambapo kwa kipindi kama hicho mashauri 97 yaliripotiwa katika ofisi ya Ustawi wa Jamii mkoa wa Songwe.